728x90 AdSpace

  • Latest News

    Thursday, July 16, 2015

    LEO ALHAMISI CECAFA KUWAPIMA WAAMUZI WATAKAOCHEZESHA KAGAME


    Baraza la Vyama Vya Soka kwa Nchi za Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) leo Alhamisi Julai 16, litaendesha mtihani wa utimamu wa mwili (Physical test) kwa waamuzi wa watakochezesha michuano ya kombe la Kag
    ame inayoanza mwishoni mwa wiki huu.

    Zoezi hilo la utimamu kwa waamuzi watakochezesha mashindano ya Kagame, litafanyika kuanzia saa 2 asubuhi katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam litasimamiwa na kamati ya waamuzi ya ya CECAFA.

    Waamuzi wanaotarajiwa kuhudhuria zoezi hilo ni Ali Ahmed, Suleiman Bashir (Somalia), Ahmed Djama (Djibout), Yetayew Belachew (Ethiopia), Kakunze Herve (Burundi), Davis Omweno, Peter Sabata (Kenya), Issa Kagabo, Hakizimana Louis (Rwanda), Ahemd El Faith (Sudan), Lee Okelo na Mashood Ssali (Uganda), Israel Mjuni na Ferdinand Chacha (Tanzania).
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: LEO ALHAMISI CECAFA KUWAPIMA WAAMUZI WATAKAOCHEZESHA KAGAME Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top