728x90 AdSpace

  • Latest News

    Sunday, July 12, 2015

    OTAMENDI MIKONONI MWA JORGE MENDEZ,PEDRO NAENDA CHELSEA MIE,CHAMBERS SIENDI SOUTHAMPTON KWA MKOPO.



    Topal:Batur Altiparmak ambaye ni wakala wa kiungo wa Fenerbahce Mehmet Topal amesema mteja wake haendi kokote licha ya kudaiwa mapema wiki iliyopita kuwa klabu ya Arsenal ilituma ofa ya €7m ili kutaka k
    umsajili nyota huyo wa zamani wa Valencia.

    Otamendi:Wakala Eugenio Lopez anayemuwakilisha mlinzi wa Valencia Nicolas Otamendi,27 ameripotiwa kumuomba wakala maarufu Jorge Mendez kumsaidia mteja wake ili aweze kutimiza ndoto ya kupata timu nchini England.

    McCarthy:Tottenham imeandaa kitita cha £25m ili kuwasajili nyota wawili mahiri wa Everton James McCarthy na Kevin Mirallas.(Daily Mirror)

    Chambers:Mlinzi wa Arsenal Calum Chambers,20 anajiandaa kukataa mpango wa kurudi kwa mkopo katika klabu yake ya zamani ya Southampton na badala yake atabakia kugombea namba.(The Sun)

    Benteke:Manchester United inaandaa kitita kikubwa cha fedha kwa ajili ya kumsajili mshambuliaji wa Aston Villa Christian Benteke,24 mwenye thamani ya £32.5m.(The Sun)

    Ashley:Mmiliki wa Newcastle United Mike Ashley amesema anaendelea kuisuka upya klabu yake na tayari ameandaa £40m kwa ajili ya kuwasajili Aleksandar Mitrovic wa Anderlecht na nyota wa Schalke Joel Matip.Hii imekuja siku moja tu tangu mmiliki huyo afanikiwe kumsajili kiungo wa PSV Georginio Wijnaldum kwa dau kubwa la £14.5m.(Daily Express)

    Delph:Kiungo wa Aston Villa Fabian Delph ameachana na mpango wa kujiunga na Man City katika siku ambayo alipaswa afanyiwe vipimo vya afya kabla ya kukamilisha usajili.Jana jumamosi nyota huyo ilikuwa afanyiwe vipimo vya afya lakini alibadili mawazo dakika za mwisho na kuamua kubakia Villa Park.(Daily Star)

    Pedro:Winga wa Barcelona Pedro Rodriquez ameripotiwa kuvutiwa kutaka kuhamia Chelsea baada ya kufanya mazungumzo ya kina na kiungo wa klabu hiyo Cesc Fabregas.(Sport)

    Levy:Mwenyekiti wa Tottenham Daniel Levy amemwambia kocha wa timu hiyo Mauricio Pochetino kuuza kwanza wachezaji sita ndipo afikirie tena kusajili nyota wapya.(Daily Express)

    Aranguiz:Chelsea inakabiriwa na upindani mkali katika kuinasa saini ya kiungo wa Chile Charlez Aranguiz hii ni baada ya vilabu vya Arsenal na Liverpool kuripotiwa kuitaka huduma ya mshindi huyo wa Copa America.(Daily Mail)

    Evans:Arsenal imeripotiwa kuandaa kitita cha £10m ili kumsajili mlinzi wa Manchester United John Evans (Mirror)

    Vidal:Juventus imetangaza kuwa klabu yoyote inayotaka kumsajili kiungo wake Arturo Vidal iandae kitita cha £32m. (Sunday Express)
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: OTAMENDI MIKONONI MWA JORGE MENDEZ,PEDRO NAENDA CHELSEA MIE,CHAMBERS SIENDI SOUTHAMPTON KWA MKOPO. Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top