MABINGWA wa Tanzania Bara,Yanga SC wamepangwa Kundi A pamoja na Gor Mahia ya Kenya,Khartoum FC ya Sudan, Telecom ya Somalia na KMKM ya Zanzibar katika
michuano ya 41 ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati,Kombe la Kagame.
Katika mkutano na Waandishi wa Habari leo makao makuu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF),Ilala, Dar es Salaam, Katibu wa CECAFA, Nicholas Musonye amesema kwamba mabingwa wa mwaka jana,Azam FC wamepangwa Kundi C pamoja na Malakia ya Sudan Kusini, KCC ya Uganda na Adama City ya Ethiopia.
Mkutano huo uliohudhuriwa na Mwenyekiti wa CECAFA,Leodegar Tenga, Rais wa TFF, Jamal Malinzi,ulishuhudia APR ya Rwanda ikipangwa Kundi B pamoja na timu za Al Shandy ya Sudan, Lydia Ludic Burundi ya Burundi na Elman ya Somalia.
Michuano hiyo inatarajiwa kufanyika mjini Dar es Salaam, Tanzania,kuanzia Jumamosi ya Julai 18 hadi Jumapili ya Agosti 2, mwaka huu.
Mabingwa watetezi, El Merreikh ya Sudan wamejitoa ili wapate fursa ya kushiriki vyema hatua ya makundi ya Ligi Mabingwa Afrika.
MAKUNDI KOMBE LA KAGAME 2015:
KUNDI A: Yanga (Tanzania), Gor Mahia (Kenya), Khartoum (Sudan),Telecom (Somalia), KMKM (Zanzibar)
KUNDI B: APR (Rwanda), Al Shandy (Sudan), LLB (Burundi), Elman (Somalia)
KUNDI C: Azam (Tanzania), Malakia (South Sudan), KCC (Uganda),Adama City (Ethiopia)
0 comments:
Post a Comment