728x90 AdSpace

  • Latest News

    Wednesday, July 01, 2015

    GERVINHO AKANA KUTAKA HELICOPTA ILI ATUE AL JAZERA

    Roma,Italia.
    Winga wa klabu ya AS Roma Gervas Yao Quasi maarufu kama Gervinho amekana kutaka apewe helicopta ili akubali kuichezea klabu ya Al Jazira ya Abu Dhabi.

    Gervinho,28 amesema
    anashangaa kusikia kuwa ameshindwa kufikia makubaliano na klabu hiyo ya falme za kiarabu kwa kuwa Al Jazira imeshindwa kumpa helicopta pamoja na kumtafutia beach ya peke yake.

    Amesema "Nasoma kuhusu helicopa,beach mara tiketi za ndege.Sijui habari hizi zinatoka wapi,sijataka vitu kama hivyo.

    "Ninaposaini kucheza huwa siangalii vitu kama hiyo;yote yaliyosemwa kuhusu mimi ni uzushi na uongo mkubwa"Alimaliza Gervinho.

    Mapema jana kuliibuka taarifa kuwa usajili wa Gervinho kwenda Al Jazira umeota mbawa baada ya nyota huyo wa zamani wa vilabu vya Arsenal na Lille kudai apewe helicopa,nyumba,ticketi za ndege na nyumba ya kuishi ndipo asaini kuichezea miamba hiyo ya Abu Dhabi.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: GERVINHO AKANA KUTAKA HELICOPTA ILI ATUE AL JAZERA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top