728x90 AdSpace

  • Latest News

    Tuesday, July 14, 2015

    DAU ALILOUZWA EMMANUEL OKWI LAWEKWA HADHARANI

    Baada ya chenga nyingi, sasa mambo yako hadharani kuwa Simba imemuuza Emmanuel Okwi kwa Sh milioni 220.

    Okwi ameuzwa katika klabu ya Sønderjysk
    E ya nchini Denmark ambayo amejiunga nayo kwa mkataba wa miaka mitano.

    Awali, Simba kupitia kaimu katibu wake mkuu, Collins Frisch ilikuwa ikifanya siri kubwa bila sababu yoyote.
    Lakini uongozi wa SønderjyskE umeweka wazi kwamba umemnunua Okwi kwa dola 110,000.

    Baadaye Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe naye amelithibitisha hilo.

    “Kweli ni fedha hizo, katikati ya mwezi huu nafikiri tarehe 17, watatulipa,” alisema.
    Tayari Okwi ameichezea timu hiyo kwa dakika 76 katika mechi ya kirafiki dhidi ya Schleswigers.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: DAU ALILOUZWA EMMANUEL OKWI LAWEKWA HADHARANI Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top