Kocha wa Arsenal Mfaransa Arsene Wenger ameonyesha kushangazwa na hatua ya Manchester United kumuuza mshambuliaji wake mahiri Robin van Persie,31 kwenda klabu ya Fenerbahce.
Akifanya mazungumzo na wanahabari wa Singapore kabla ya mchezo wa kesho jumamosi wa fainali wa kombe la Barclays Asia Trophy,Wenger amesema
"Ni pigo kubwa kwa soka la Uingereza kwa sababu Robin bado ni mchezaji mzuri.Ni mmoja kati ya wachezaji wazuri sana niliowahi kuwafundisha,ni mchezaji mwenye kipaji cha kipekee.
"Sijui ni nini kimetokea,sijui kwanini ameamua kuhama Manchester United.Kuondoka kwake ni pigo mno"
Wenger alimnunua Van Persie kutoka Feyenoord ya Uholanzi kwa £2.75m mwaka 2004, kabla ya kumuuza mwaka 2012 kwenda Manchester United kwa £25m.
0 comments:
Post a Comment