728x90 AdSpace

  • Latest News

    Sunday, July 12, 2015

    YANGA YAIPIGA POLISI KOMBAINI 3-0,NGOMA AENDELEA KUTUPIA

    Mabingwa wa ligi kuu Tanzania bara klabu ya Yanga, leo imefanikiwa kuibuka na ushindi mnono baada ya kuitandika timu ya Polisi Kombaini kwa magoli 3-0 kwenyemchezo wa kirafiki wa kujipima nguvu uliopigwa kw
    enye uwanja wa Taifa jijini Dares Salaam jioni ya leo.

    Magoli ya Yanga yamefungwa na Simon Msuva dakika ya 28, Amis Tambwe dakika ya 33 na mshambuliaji mpya wa klabu hiyo aliyesajiliwa kutoka klabu ya FC Platinum ya Zimbabwe Donald Ngoma ambaye amepigilia msumari wa mwisho dakika ya 75 na kuipa timu yake ushindi huo maridhawa.

    Mchezo huo ni moja ya maandalizi kwa klabu ya Yanga kuelekea kwenye michuano ya Kagame inayotarajia kuanza kutimua vumbi Agosti 18 mwaka huu jijini Dar es Salaam.

    Kikosi hicho cha wanajangwani kinatarajia kuingia kambini kesho (Jumatatu) kwa ajili ya kuendelea kujifua kujiandaa na mashindano hayo ya Kagame yanayoshirikisha vilabu bingwa vya ukanda wa Afrika Mashariki na Kati

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: YANGA YAIPIGA POLISI KOMBAINI 3-0,NGOMA AENDELEA KUTUPIA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top