728x90 AdSpace

Monday, July 13, 2015

MAN UNITED YAZIDI KUNOGA,SCHNEIDERLIN ASAINI MIAKA MINNE,TIMU KWENDA MAREKANI LEO MCHANA!!



Klabu ya Manchester United imeendelea kuonyesha umwamba wake katika dirisha la usajili baada ya kudaiwa kufanikiwa kuinasa saini ya kiungo wa Southampton Morgan Schneiderlin kwa ada ya £25m.

Schneiderlin,25 alikamilisha vipimo vyake vya afya jana jioni na leo anatarajiwa kusaini mkataba wa miaka minne utakaomuwezesha kuvuna mshahara wa £100,000 kwa wiki.

Wakati huo huo Manchester United inatarajiwa leo mchana kuelekea nchini Marekani kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya wa ligi kuu ya EPL.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 comments:

Post a Comment

Item Reviewed: MAN UNITED YAZIDI KUNOGA,SCHNEIDERLIN ASAINI MIAKA MINNE,TIMU KWENDA MAREKANI LEO MCHANA!! Rating: 5 Reviewed By: Unknown