Mama mzazi wa mlinda mlango Iker Casillas aitwaye Carmen Fernandez amemshambulia rais wa klabu ya Real Madrid Florentino Perez kwa kumuuza kwa nguvu mwanae kwenda klabu ya F
C Porto ya Ureno.
Carmen ambaye alikuwa sehemu ya umati uliokuja kumuaga mwanae wakati akitangaza kuihamu klabu hiyo amesema
"Mwanangu alikuwa na ofa nyingi lakini Perez hakutaka Iker ajiunge na klabu kubwa. Hakutaka Iker afanikiwe.Mwanangu siyo mtu wa kwenda kucheza klabu kama Porto wakati kuna vilabu vikubwa vilikuwa vikimtaka.Iker anauzwa kibabe licha ya kuifanyia mambo mengi mazuri klabu hii.Perez ni mtu mbaya"
0 comments:
Post a Comment