728x90 AdSpace

  • Latest News

    Thursday, July 16, 2015

    DRAXLER JUVENTUS VIDAL BAYERN,ABRAMOVIC AENDA URUSI KUMLETA AXEL WITSEL,KIKO CASILLA MIKONONI MWA MADRID

    Robinho:Winga Mbrazil Robinho amejiunga na klabu ya Guangzhou Evergrande ya China kwa mkataba wa miezi sita akitokea klabu ya Santos.Robinho anakuwa mchezaji wa pili toka Brazil kutua klabuni hapo baada ya Paulinho kujiunga na miaka hiyo mwezi uliopita.

    Witsel:Chelsea imepania kumsajili kiungo mahiri wa Zenit St Petersburg Axel Witsel mwenye thamani ya £28m na tayari mmiliki wa klabu hiyo Roman Abramovic amesafiri kwenda Urusi kufanya mazungumzo na viongozi wa Zenit.(The Sun)

    Casilla:Real Madrid inakaribia kumsajili mlinda mlango wa Espanyol Kiko Casilla kwa ada ya €7m.Casilla,27 anarejea Real Madrid kuziba nafasi iliyoacha wazi na mlinda mlango Ike Casillas aliyeenda FC Porto.Kiko Casilla aliwahi kucheza Madrid kabla ya kuuzwa mwaka 2007.(AS)

    Vidal:Bayern Munich imeripotiwa kuwa karibu kuinasa saini ya kiungo wa Juventus Arturo Vidal 28 baada ya baada ya ofa yake ya £28m kukubaliwa na miamba hiyo ya Seria A.Taarifa za ndani zinasema Bayern itampa Vidal mkataba wa miaka mitano na mshahara wa £86,000 kwa wiki.(Gazzetta dello Sport)

    Rugani:Arsenal imeripotiwa kutuma ofa ya £15.4m kwenda Juventus kwa ajili ya kumsajili mlinzi kinda wa klabu hiyo Daniele Rugani,20.

    Lacazette:Rais wa Lyon Jean-Michel Aulas ameviambia vilabu vya Arsenal na Chelsea £35m itatosha kuinasa saini ya mshambuliaji hatari wa klabu hiyo Mfaransa Alexandre Lacazette,24.

    Draxler:Juventus inataka kumsajili kiungo wa Shalke O4 Julian Draxler,21 kama mbadala wa viungo wanaotaka kutimka klabuni hapo Arturo Vidal na Paul Pogba.(Gazetta dello Sport)





    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: DRAXLER JUVENTUS VIDAL BAYERN,ABRAMOVIC AENDA URUSI KUMLETA AXEL WITSEL,KIKO CASILLA MIKONONI MWA MADRID Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top