728x90 AdSpace

  • Latest News

    Wednesday, July 08, 2015

    CRYSTAL PALACE KUMSAJILI CABAYE KWA DAU LA REKODI,MAN UNITED YAKUBALI KUMUUZA DE GEA,CHELSEA YAMNASA ARANGUIZ



    De Gea:Kutoka gazeti la El Confidencial la Hispania habari zinasema Manchester United imekubali kumuuza mlinda mlango wake David De Gea kwenda Real Madrid kwa dau la £28.6m na tayari mkataba wa miaka sita umeshaandaliwa kwa ajili yake.
    Cabaye:Crystal Palace huenda ndani ya saa 48 zijazo ikaweka rekodi ya usajili kwa kumsajili Yohan Cabaye toka PSG kwa ada ya £10m ambayo itapanda mpaka £13m.Ikiwa usajili huo utakamilika hiyo itakuwa ni ada kubwa zaidi kuwahi kutolewa na Palace katika usajili.(BBC)
    Tokeo la picha la andrea pirlo
    Pirlo:New York City FC imesema haitamtoa kwa mkopo nyota wake Andrea Pirlo 36 kwenda Manchester City kama ilivyofanya msimu uliopita kwa Frank Lampard.(ESPN)
    Kenedy:Chelsea iko mbioni kukamilisha usajili wa kinda wa Fluminense aitwaye Kenedy.Habari za kuaminika zinasema kinda huyo mwenye thamani ya £6.3m ameshafanya vipimo vya afya na muda wowote kuanzia sasa atatangazwa kuwa mchezaji mpya wa Chelsea.
    Tokeo la picha la di maria
    Di Maria:Bayern Munich imeripotiwa kuwa katika mazungumzo na Manchester United kwa ajili ya kubadirishana wachezaji Angel Di Maria na Mario Gotze au Sebastian Schweinsteiger.(Bild)
    Fekir:Arsenal imepata pigo katika mbio za kumfukuzia  kiungo wa Lyon Nabil Fekir 21 baada ya nyota huyo Mfaransa kusaini mkataba mpya wa kuendelea kukipiga Stade de Gerland.
    Aranguiz:Kutoka Chile habari zinasema Chelsea iko katika nafasi nzuri ya kumsajili nyota wa Internacional ya Brazil na timu ya taifa ya Chile Charles Aranguiz 26 baada ya kukubali kutoa kitita cha £18m.
    \
    Ruiz:Sporting Lisbon imemsajili mshambuliaji wa Fulham na timu ya taifa ya Costa Rica Bryan Ruiz.Ruiz 29 amesaini mkataba wa miaka mitatu wa kuichezea miamba hiyo ya Ureno huku kukiwa na kipengele cha kuuzwa kwa €60 million (£43m).
    Darmian:Mlinzi wa Torino Matteo Darmian muda mfupi ujao atatua London kabla ya kuelekea Manchester kukamilisha taratibu za kujiunga na Manchester United.(Tuttosport)







    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: CRYSTAL PALACE KUMSAJILI CABAYE KWA DAU LA REKODI,MAN UNITED YAKUBALI KUMUUZA DE GEA,CHELSEA YAMNASA ARANGUIZ Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top