728x90 AdSpace

  • Latest News

    Wednesday, July 01, 2015

    BLATTER AKACHA FAINALI YA KOMBE LA DUNIA LA WANAWAKE

    Tokeo la picha la blatter
    Rais wa shirikisho la soka duniani (FIFA) Sepp Blatter hatohudhuria kwenye mchezowa fainali wa kombe la dunia la wanawake 2015
    mchezo utakaopigwa Vancouver, British Columbia, Blatter hatohudhuria fainali hiyo kutokana na sababu zake binafsi.

    Kiutamaduni, rais wa FIFA ndiye anaetakiwa  akabidhi  kombe la dunia kwa mshindi wa fainali hiyo ya wanake, lakini mwaka huu haitakuwa hivyo. Imeripotiwa na shirika la habari la Uingereza Reuters kwamba, mwanasheria mkuu wa FIFA Richard Cullen amethibitisha habari hizo akisema:

    Hatokuwepo kwenye mchezo wa fainali Canada. Amewataarifu waratibu wa michuano hiyo na amesema ana sababu zake binafsi za kutohudhuria”.

    Hii itakuwa ni mara ya kwanza kutokea tangu Blatter aanze kuiongoza FIFA kutohudhuria sherehe za fainali za kombe la dunia. Kwa mujibu wa mwandishi wa habari za michezo Ker Radnedge, katibu mkuu wa FIFA Jerome Valcke pia hatokuwepo Canada.

    FIFA imesema sababu za kutokuwepo kwao ni kutokana na wote kuakabiliwa na majukumu huko Zurich.Mwandishi wa BBC (BBC Sports) Natalie Pirks ameandika kwenye account yake ya twitter akilaumu baada ya kusikia habari kwamba Blatter hatohudhuria kwenye fainali hiyo.

    Blatter amethibitisha atajiuzulu nafasi yakeya urais wa FIFA baada ya uchunguzi wa maafisa wa Kimarekani kubaini kuwepo na sakata la rushwa ndani ya FIFA na kuwakamata baadhi ya maafisa wa shirikisho hilo.

    Mwandishi wa The Guardian Owen Gibson amehoji kwamba, Tangu uchunguzi huo uwekwe hadharani, Blatter amekuwa hasafiri tena mara kwa mara, ni rahisi kujuani kwanini.Gibson ameripoti kwamba, Blatter pia anafanyiwa uchunguzi na shirika la Kimarekani la FBI akituhumiwa kwa matukio ya rushwa na ubadhilifu wa pesa yanayo ikabili FIFA lakini mamlaka za Uswis tayari zimethibitisha kwamba, Blatter hayupo kwenye watu wanaofanyiwauchunguzi na mamlaka hizo.

    Watu wengi wamekuwa wakisema kuwa, Blatter huenda anahofia kukamatwa pindi atakapo safiri kwenda Canada. Lakini kutokuwepo kwake kwenye fainali ya kombe la dunia la wanawake hakutatoa picha nzuri.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: BLATTER AKACHA FAINALI YA KOMBE LA DUNIA LA WANAWAKE Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top