728x90 AdSpace

  • Latest News

    Tuesday, July 07, 2015

    AZAM FC DIMBANI LEO KUJIPIMA UBAVU NA MAAFANDE WA JKT RUVU



    Azam FC inatarajia kucheza mechi ya kirafiki na JKT Ruvu kwenye Uwanja wa Azam Complex , mchezo ambao kocha Stewart Hall atautumia kuwapima wachezaji wake akiwemo mlinda
    Mlango Muivory Coast, Vincent Atchouailou de Paul Angban.

    Kwa mujibu wa habari kutoka katika mtandao wa klabu ya Azam FC, Vincent ametua Dar es Salaam wikiendi iliyopita na leo Jumanne atacheza mchezo huo wa kwanza kwenye kikosi cha Azam na JKT inayonolewa na kocha, Fred Minziro. 

    Kocha wa Azam, Muingereza Hall amesema mechi hiyo itakuwa ni ajili ya kujipima.

    "Katika mchezo huo, natarajia kumtumia kipa Muivory Coast aliyewasili wikiendi hii kwa majaribio.", amenukuliwa Hall akisema.

    Huo ni mchezo wa pili wa Azam wa kirafiki baada ya ule wa kwanza wa wiki iliyopita, waliocheza na France Rangers wakashinda 4-2. Azam inajiandaa na michuano ya Kombe la Kagame itakayofanyika Dar es Salaam baadae mwezi huu.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: AZAM FC DIMBANI LEO KUJIPIMA UBAVU NA MAAFANDE WA JKT RUVU Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top