728x90 AdSpace

  • Latest News

    Saturday, July 04, 2015

    STARS YAAGA MICHUANO YA CHAN,YATOKA SARE YA 1-1 NA UGANDA

    Timu ya taifa ya Tanzania "Taifa Stars" imetupwa nje ya michuano ya kusaka tiketi ya kushiriki michuano ya Afrika ya wachezaji wa ndani maarufu kama CHAN.

    Stars ambayo wiki mbili zilizopita ilikubali kichapo cha goli 3-0 dhidi ya Uganda leo jioni imejitutumua na kutoka sare ya goli 1-1 katika mchezo mkali ulipigwa katika dimba la Nakivuko jijini Kampala.Stars ilipata goli lake kwa mkwaju wa penati uliopigwa na mshambuliaji wake mrefu John Raphael Bocco kabla ya wenyeji Uganda kusawazisha kupitia kwa Kezironi Kizito.

    Kufuatia matokeo hayo Uganda inasonga mbele kwa ushindi wa jumla ya goli 4-1.Uganda itavaana na Sudan kabla ya kukata tiketi ya kufuzu ya michuano hiyo itakayopigwa nchini Rwanda mwaka 2016.

    Uganda Cranes XI:
    James Alitho (GK), Denis Okot Oola, Brian Ochwo, Hassan Waswa Mawanda (Captain),Shafiq Bakaki, Derick Tekkwo, Muzamil Mutyaba, Erisa Sekisambu, Farouk Miya, John Semazi, Robert Sentongo.

    Tanzania XI:
    Ally Mustafa Mtinge (G.K), Nadir Haroub Ali,John Raphael Bocco, Salum Shomari Kapombe, Frank Domayo Raymond, Saimon
    HappyGod Msuva, Kelvin Patrick Yondani,Mwinyi Haji Mngwali, Rashid Y. Mandawa,Deus Kaseke David, Abbas Mudathiri Yahya.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: STARS YAAGA MICHUANO YA CHAN,YATOKA SARE YA 1-1 NA UGANDA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top