728x90 AdSpace

  • Latest News

    Saturday, July 18, 2015

    ROMA YAIGONGA REAL MADRID 7-6,GERVINHO AFUNIKA VIBAYA.

    Rafa Benitez ameanza vibaya kibarua cha kuinoa Real Madrid baada ya kuishuhudia klabu hiyo ikipata kichapo cha penati 7-6 toka kwa Roma ya Italia katika mchezo ulioisha hivi punde wa michuano ya Gold Cup 2015.

    Katika mchezo huo uliopigwa huko Melbourne,Australia katika dimba la MGM lililokuwa limesheheni watazamaji 80,000 ilishuhudiwa mpaka dakika 90 zinaisha miamba hiyo ikiwa sare ya 0-0 na mwamuzi kuamua ipigwe mikwaju ya penati na Roma kuibuka washindi.

    Pongezi za dhati zimuendee kipa wa Roma Morgan De Sanctis kwa kudaka penati ya Lucas Vasquez kabla ya kiungo Seydou Keita kufunga penati ya mwisho na kuipa Roma ushindi wa penati 7-6.

    Wakati huo huo winga wa Roma Gervinho ametwaa tuzo ya mchezaji bora wa mechi hiyo baada kuonyesha soka safi.

    Real Madrid itashuka dimbani siku ya ijumaa kuivaa Manchester City huku Roma na Manchester City wakivaana siku ya jumanne.

    Katika mchezo mwingine Manchester City iliifunga Melbourne FC goli 1-0.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: ROMA YAIGONGA REAL MADRID 7-6,GERVINHO AFUNIKA VIBAYA. Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top