728x90 AdSpace

  • Latest News

    Monday, July 06, 2015

    AZAM FC DIMBANI KESHO DHIDI YA JKT RUVU

     
    Azam FC inatarajia kucheza mechi ya kirafiki na JKT Ruvu kwenye Uwanja wa Azam Complex kesho Jumanne saa 10 jioni, mchezo
    ambao kocha Stewart Hall atautumia kuwapima wachezaji wake akiwemo mlinda Mlango Muivory Coast, Vincent Atchouailou de Paul Angban.

    Vincent ametua Dar es Salaam wikiendi iliyopita na Jumanne atacheza mchezo huo wa kwanza kwenye kikosi cha Azam na JKT inayonolewa na kocha, Fred Minziro.


    Stewart alisema: "Tunaendelea vizuri na mazoezi na Jumanne tutacheza mechi ya kirafiki na JKT kwa ajili ya kujipima. Katika mchezo huo, natarajia kumtumia kipa Muivory Coast aliyewasili wikiendi hii kwa majaribio."


    Huo ni mchezo wa pili wa Azam wa kirafiki baada ya ule wa kwanza wa wiki iliyopita, waliocheza na France Rangers wakashinda 4-2
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: AZAM FC DIMBANI KESHO DHIDI YA JKT RUVU Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top