Baada ya kuanza vema mechi zao za
michuano ya vilabu barani Afrika, makocha wa wawakilishi wa Tanzania,
Azam FC na Yanga wamesema kuwa wana matumaini ya kusonga mbele katika
mechi zao za marudiano zitakazofanyika baada ya wiki mbili mjini
Khartoum (Sudan) na Gaborone (Botswana).
Yanga, wawakilishi wa
Tanzania katika
michuano ya kombe la Shirikisho Afrika (CAF
Confederation Cup) waliwafunga BDF XI ya Botswana 2-0 na kocha wa Yanga,
Mdachi Hans Van de Pluijm amesema amefurahishwa na ushindi huo na
kusema anahitaji goli moja tu au zaidi katika mechi ijayo ili timu yake
isonge mbele.
“Tunahitaji ushindi mdogo au sare ya kutokufungana ili tusonge mbele”,
“Tumeweza
kuutumia vyema uwanja wa nyumbani na tunahitaji ushindi mwingine ili
tufanikiwe”, alisema Pluijm, huku amkimsifia Mrundi Amisi Tambwe kwa
kufunga magoli yote.
Naye kocha wa Azam, Mcameroon, Joseph Omog amekisifu kikosi chake kwa kuwafunga El-Merreikh ya Sudan 2-0.
“Tunakazi
ngumu mechi ya marudiano kwa kuwa wapinzani wetu ni wazuri na watakuwa
wakicheza nyumbani, ila tunajitahidi ili tuweze kufunga zaidi ili
tusonge mbele.
Azam ni mara ya kwanza kushiriki michuano ya ligi
ya Mabingwa Afrika huku Yanga, iliyofikisha miaka 80 mwezi Februari
mwaka huu tangu ilipoanzisha, ikiwa na uzoefu wa kutosha.
0 comments:
Post a Comment