London,England.
Kocha Jose Mourinho ameibuka na kudai kuwa chama cha soka cha Ufaransa FFF kinapaswa kumwandikia barua ya kumwambia asante baada ya kuwaibua walinzi Raphael Varane na Kurt Zouma.
Akifanya mahojiano na waandishi wa habari kabla ya mchezo wa kesho wa ligi kuu dhidi ya Aston Villa,Mourinho maarufu kama Special One hakuacha kujisifia kama ilivyo kawaida yake baada ya kusema ..
"Chama cha soka cha Ufaransa kinapaswa kunipongeza kwa kazi nzuri.Nimewaibua Kurt Zouma na Raphael Valane,hakuna aliyewajua kabla leo hii ni walinzi mahiri duniani"
Akiwa katika klabu ya Real Madrid Mourinho alimsajili Valane kutoka klabu ya Lens akiwa na miaka 18 tu mwaka 2011 na kuanza kumtumia katika mechi mbali mbali kabla ya mwaka jana kumsajili Zouma toka klabu ya St Ettiene kwa ada ya £12m na tayari ameshaanza kumwamini na kumpa nafasi kikosi cha kwanza.
0 comments:
Post a Comment