728x90 AdSpace

  • Latest News

    Monday, February 02, 2015

    USAJILI:MANCHESTER UNITED YATENGA €90M KUWANASA DE BRUYNE NA HUMMELS

    Olinga:Klabu ya Chelsea imeripotiwa kuanza kumtupia macho kinda Mcameroun wa klabu ya Malaga Fabrice Olinga 18 baada ya Samwel Eto'o kumpeleka kufanya majaribio katika klabu ya Sampdoria.

    Marquinhos:Klabu ya Paris Saint Germain imeripotiwa kukataa ofa ya €45m toka klabu ya Manchester United kwa ajili ya mlinzi wake Marquinhos.

    Mirallas:Klabu ya Tottenham inajiandaa kupeleka kitita cha £5m pamoja na winga wake Aaron Lenon kwa ajili ya kumsajili nyota wa Everton Kevin Mirallas.

    Tiote:Klabu ya Locomotiv Moscow imeripotiwa kuwa katika pilika pilika za kutaka kumsajili kiungo wa klabu ya Newcastle Cheik Tiote kwa ada inayodhaniwa kuwa ni kati ya €13-16m.

    Manchester United:Klabu ya Manchester United imeripotiwa kutenga kitita cha €90m kwa ajili ya kufanya usajili wa kushitukiza wa nyota wa Bundesliga Kevin de Bruyne na Mats Hummels.

    Santon:Klabu ya Inter Milan imeripotiwa kuwa katika hatua za mwisho za kumnasa nyota wake wa zamani mlinzi Davide Santon anayekipiga katika klabu ya Newcastle United kwa uhamisho wa mkopo wa miezi sita.

    Cassano:Mshambuliaji mtukutu Antonio Cassano ameripotiwa kukataa kujiunga na klabu ya QPR ili ajiunge na klabu ya Inter Milan.

    N'doye:Klabu ya Hull City iko katika hatua za mwisho za kukamilisha usajili wa nyota wa klabu ya Lokomotiv Moscow Dame N'Doye kwa kitita cha £4m. 


    Gomis:Klabu ya Swansea City imekataa ofa ya £7m toka klabu ya Westham kwa ajili ya mshambuliaji wake Mfaransa Bafetimbi Gomis.

    Adebayor:Mshambuliaji wa Tottenham Emanuel Adebayor amekataa ofa ya kujiunga na klabu ya QPR kwa mkopo licha ya vilabu vyote viwili kuripotiwa kufikia makubaliano.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: USAJILI:MANCHESTER UNITED YATENGA €90M KUWANASA DE BRUYNE NA HUMMELS Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top