728x90 AdSpace

  • Latest News

    Monday, February 23, 2015

    CHELSEA KUMKATIA RUFAA NEMANJA MATIC

    London,England.

    Chelsea wako njiani kuipinga Kadi nyekundu aliyopewa Kiungo wao Nemanja Matic hapo Jumamosi walipotoka Sare 1- 1 na Burnley kwenye Mechi ya Ligi Kuu England.
     
    Matic, Kiungo wa miaka
    26 kutoka Serbia alitolewa nje kwa Kadi Nyekundu katika dakika ya 70 alipomsukuma na kumwangusha Ashley Barnes ambae alimchezea rafu mbaya.
    Chelsea wamepewa hadi Jumanne Saa 10 Jioni kuwasilisha ushahidi wa Rufaa yao kwa FA, Chama cha Soka England.

    Endapo Chelsea hawatakata Rufaa basi Matic ataikosa Fainali ya Capital One Cup dhidi ya Tottenham hapo Jumapili na pia kuzikosa Mechi za Ligi dhidi ya West Ham na Southampton.

    Katika Gemu hiyo ya Jumamosi , Burnley walisawazisha Bao katika dakika ya 81 na mchezo kwisha 1- 1 lakini Mourinho alidai Barnes hakupaswa kuwepo Uwanjani wakati anafarakana na Matic kwani katika dakika ya 31 alimchezea Rafu mbaya Branislav Ivanovic ambayo ilistahili Kadi nyekundu.

    Mbali ya tukio hilo pia Mourinho alilalamikia kumyimwa Penati 2 na refa Martin Atkinson wakati Michael Kightly alipounawa Mpira Dakika ya 34 na Jason Shackell kumchezea Rafu Diego Costa katika dakika ya 44 .

    Huku akiogopa kuadhibiwa tena na FA kwa kukashifu Marefa, Mourinho alipanga maneno yake vizuri pale alipomponda Refa Martin Atkinson kwa kusema : “ Gemu hii ilikuwa na matukio muhimu Manne katika dakika za 30, 33 , 43 na 69 . Hii ndio hadithi ya hii Gemu . Siwezi kuongea zaidi ” kwasababu ni ngumu kwangu kutosema ukweli !

    Cha ajabu ni kuwa huko nyuma, Meneja wa Manchester United Sir Alex Ferguson,alishawahi kulalamika kuwa refa Martin Atkinson ‘ huibeba ’ Chelsea kila
    wanapocheza nayo kitu ambacho kilimtia matatani na FA licha ya Rekodi kuonyesha refa akiichezesha Chelsea huwa haifungwi .
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: CHELSEA KUMKATIA RUFAA NEMANJA MATIC Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top