728x90 AdSpace

  • Latest News

    Monday, February 02, 2015

    BONY,GERVINHO WAIPELEKA IVORY COAST NUSU FAINALI AFCON

    Malabo,Guinea.

    Magoli mawili ya mshambuliaji Wilfred Bony na moja la winga Gervais Yao Gervinho dhidi ya Algeria yametosha kuipeleka Ivory Coast katika hatua ya nusu fainali ya michuano ya Afcon.

    Ivory Coast ndiyo waliokuwa wa kwanza kuamsha mashabiki wao katika uwanja wa Estadio Malabo baada ya mpira wa adhabu uliopigwa na kiungo Yaya Toure kutua kichwani mwa Bony na kuandika bao.

    Baada ya bao hilo Algeria waliamka na kupata bao la kusawazisha kupitia kwa mshambuliaji wao mahiri El Arabi Hilal Soudani,Ivory Coast ikaongeza kupitia Bony kabla ya Gervinho kufunga la tatu.

    Ratiba ya nusu fainali iko kama ifuatavyo....

    4/02/2015 Congo v Ivory Coast

    5/02/2015 Ghana v Guinea

    Mechi zote zitapigwa saa 4:00 usiku.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: BONY,GERVINHO WAIPELEKA IVORY COAST NUSU FAINALI AFCON Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top