Mshambuliaji wa kimataifa wa Burundi, Amisi Tambwe leo ameibuka
shujaa katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam baada ya kuifungia
timu yake ya Yanga magoli na kuifanya timu hiyo kuibuka na ushindi hu wa
2-0 dhidi ya BDF XI ya nchini Botswana.
Yanga na BDF XI zimekutana leo kwenye mchezo wa
kwanza wa Raundi ya awali ya kombe la shirikisho la soka barani Afrika.
kwanza wa Raundi ya awali ya kombe la shirikisho la soka barani Afrika.
Wachambuzi wa soka wanaelezea kuwa ushindi huo wa
magoli 2-0 unaiweka timu ya Yanga katika nafasi nzuri ya kuweza kuingia
hatua ya 32 bora.
Tambwe aliipatia timu yake goli la kwanza katika
dakika ya kwanza kwa kichwa akiunganisha krosi nzuri iliyopigwa na
winga machachari Simon Msuva huku mabeki wa BDF XI wakibaki wanashangaa.
Goli hilo lilidumu hadi kipindi cha kwanza ndipo
tena Tambwe alipoibuka tena katika dakika ya 55 akiifungia timu yake
goli la pili kwa kichwa baada ya kuunganisha krosi nzuri kutoka kwa
Mrisho Ngassa.
0 comments:
Post a Comment