London,England.
Klabu ya Tottenham Hotspurs imeendelea kuwa moto katika uwanja wake wa nyumbani wa White Hart Lane baada ya leo hii kuinyuka Arsenal kwa magoli 2-1.
Arsenal ndiyo ilikuwa ya kwanza kupata bao dakika ya 11 kupitia kwa kiungo Mesut Ozil baada ya kazi nzuri ya mshambuliaji Danny Welbelk aliyemzidi mbio mlinzi Danny Rose na kupiga krosi iliyopalazwa na Olivier Giroud kabla ya kumkuta Mjerumani huyo na kuutia mpira kimiani.
Spurs iliyokuwa imeutawala mchezo ilipata goli lake la kwanza kupitia kwa Harry Kane dakika ya 79 kabla ya kuongeza la pili dakika ya 86.
Kufuatia matokeo hayo Spurs imepanda mpaka nafasi ya nne ikiwa na pointi 43 huku Arsenal ikishuka mpaka nafasi ya sita ikiwa na pointi 42.
0 comments:
Post a Comment