London,England.
Kiungo wa klabu ya Arsenal Aaron Ramsey ameendelea kuipa wakati mgumu klabu hiyo baada ya kuripotiwa kuwa nje ya uwanja kwa wiki nne tena.
Ramsey 24 shujaa wa Arsenal wa msimu uliopiwa alitolewa
dakika ya tisa tu ya mchezo wa jana jumanne wa ligi kuu dhidi ya Leceister City baada ya kuumia misuli.
Ramsey ambaye alirejea uwanjani hivi karibuni baada ya kuwa nje kwa wiki sita kwa tatizo la misuli ataukosa mitanange ya hatua ya mtoano ya ligi ya mabingwa dhidi ya klabu ya Monaco ya Ufaransa.
Habari njema kwa Arsenal ni kuwa nyota Alexis Sanchez ambaye pia aliumia na kulazimika kutolewa dakika ya 68 ameripotiwa kuwa katika hali nzuri japo huenda asishuke dimbani kuivaa Middlesbrough jumapili hii katika mchezo wa kombe la FA.
0 comments:
Post a Comment