728x90 AdSpace

  • Latest News

    Monday, February 23, 2015

    BARNES AIKWEPA ADHABU YA FA

    Mshambuliaji wa Burnley Ashley Barnes hatokabiliwa na adhabu yoyote kutoka  FA kwa jinsi alivyomkabili Nemanja Matic katika mchezo ulioishia kwa sare ya 1-1 na Chelsea.
                                                       30 ashley barnes striker 30 ashley barnes striker 33 steven
    Barnes aliupata mpira, lakini alimkwatua
    Matic kwenye ugoko huku njumu zake zikiwa juu.
    Matic alioneshwa kadi nyekundu kwa kukasirishwa na tukio hilo na kumsukuma Barnes, ambaye hakuadhibiwa na mwamuzi. 

    "FA inathibitisha kuwa hakuna hatua zaidi itachukuliwa kwa Ashely Barnes kwa jinsi tukio lilivyoonekana na waamuzi," kimesema chama cha soka cha England FA. 

    FA imetoa maelekezo kupitia twitter kuzungumzia sababu za uamuzi huo  waliofikia.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: BARNES AIKWEPA ADHABU YA FA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top