London,England.
Kocha wa klabu ya Chelsea Mreno Jose Mourinho amesema mbio za ubingwa wa ligi kuu bado ziko wazi licha ya timu yake kuwa kileleni kwa pointi saba zaidi dhidi ya klabu inayoshika nafasi ya pili ya Manchester City.
Akiongea baada ya kuiongoza klabu yake kuibuka na ushindi wa goli 2-1 dhidi ya Aston Villa katika dimba la Villa Park,Mourinho amekataa kuamini kuwa kazi iliyobaki kwake na vijana wake ni ndogo.
Amesema "Kwenye nchi nyingine ningesema safi lakini hapa pointi saba siyo kitu.Hapa kila mchezo ni mgumu na lolote linaweza kutokea"
"Pointi saba ina maanisha pointi saba,tuna michezo 14 mkononi.Hapa tunaongelea pointi 42.Katika pointi hizo 42 tuko juu kwa pointi saba hiyo bado siyo kitu"
"Sishangazwi na chochote.Katika nchi hii kila timu inaweza kuchukua pointi popote hivyo ni mapema sana kuuota ubingwa".
0 comments:
Post a Comment