728x90 AdSpace

  • Latest News

    Sunday, February 01, 2015

    SAMATTA AISUBIRI TIKETI YA CSKA MOSCOW

    Mshambuliaji wa TP Mazembe, Mbwana Samatta amesema amefuzu majaribio kwenye klabu ya CSKA Moscow ya Urusi ila anasubiri majibu ya lini atajiunga nayo.

    Samatta aliyekwenda kufanya majaribio kwa wiki mbili kwenye klabu hiyo ambako alikumbana na balaa la kuumia enka na kushindwa kucheza baadhi ya mechi, ingawa amesema ana matumaini ya kufanya vizuri.

    Mshambuliaji huyo wa Taifa Stars alisema maofisa wa CSKA walimwambia kuwa watamtumia majibu ya majaribio yake kwa njia ya mtandao kati ya jana,
    Jumamosi ama mwanzoni mwa wiki ijayo.

    “Mambo yalikwenda vizuri, nilifanya majaribio kwa siku zote kama ilivyopangwa licha ya kwamba nilishindwa kucheza baadhi ya mechi,nasubiri majibu.

    “Maofisa wa pale na wakala wangu wameniambia kuwa majibu yatatoka kati ya kesho, Jumamosi ama ndani ya siku hizi mbili, nasubiri na nina imani yatakuwa mazuri,” alisema Samatta.

    Hata hivyo, taarifa zilizopatikana mjini Lubumbashi zinaeleza kuwa endapo CSKA haitatoa ofa ya nguvu kuna uwezekano mkubwa mmiliki wa Mazembe, Moise Katumbi akagoma kumruhusu Samatta hadi mkataba wake utakapomalizika.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: SAMATTA AISUBIRI TIKETI YA CSKA MOSCOW Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top