London,England.
Na Paul Manjale.
Na Paul Manjale.
Ilikuwa ni mwaka 1979 ambapo vilabu vya Arsenal,Manchester United na Liverpool kwa pamoja vilipata nafasi ya kutinga katika hatua ya robo fainali ya michuano ya kombe la FA.
Mchezo wa fainali wa kombe la FA mwaka 1979 |
Sasa ni miaka 36 tangu miamba hiyo ifanye hivyo,kinachonogesha zaidi michuano ya safari hii ni haya yafuatayo....
Arsenal ambao ni mabingwa
watetezi wa michuano hiyo baada ya kuizidi ujanja dakika za mwisho klabu ya Hull City na kuibamiza magoli 3-2 inataka kurudia historia ya mwaka 1979 pale Wembley pale ilipoibuka na ushindi wa goli 3-2 dhidi ya klabu ya Manchester United kwa goli la ushindi la nyota wake Alan Sunderland.
watetezi wa michuano hiyo baada ya kuizidi ujanja dakika za mwisho klabu ya Hull City na kuibamiza magoli 3-2 inataka kurudia historia ya mwaka 1979 pale Wembley pale ilipoibuka na ushindi wa goli 3-2 dhidi ya klabu ya Manchester United kwa goli la ushindi la nyota wake Alan Sunderland.
Huku pia ikiwa na kumbukumbu ya kutwaa taji hilo kwa mara nyingine mbele ya Manchester United mwaka 2005 kwa mikwaju ya penati baada ya dakika 120 kuisha bila ya kufungana.
Manchester United ambayo imefuzu baada ya jana usiku kuinyuka klabu ndogo ya Preston North End kwa magoli 3-1 inahitaji kushinda taji hilo kongwe zaidi katika historia ya soka la England.
Ikiwa haina uhakika kwa kutwaa taji la ligi kuu,ikiwa nje ya michuano ya Capital One pamoja na ligi ya mabingwa (UEFA),ikiwa imetangaza hasara kubwa hivi karibu Manchester United inahitaji taji hili ili kurekebisha hali ya mambo.
Liverpool inataka kushinda taji hili kwa ajili ya mashabiki na kiungo wake Steven Gerrard (35) anayetimka klabuni hapo.Gerrard atakuwa anatimiza miaka 36 mei 30 ambayo itakuwa ni siku ya fainali ya kombe hilo.
Droo kamili iko kama ifuatavyo....
Liverpool v Blackburn
Bradford v Reading
Manchester United v Arsenal
Aston Villa v West Brom
Bradford v Reading
Manchester United v Arsenal
Aston Villa v West Brom
Michezo hiyo itapigwa tarehe 7 na 8 ya mwezi machi mwaka huu.
0 comments:
Post a Comment