728x90 AdSpace

  • Latest News

    Wednesday, February 04, 2015

    VPL:YANGA YAIFUNGA COASTAL,CANNAVARO SHUJAA

    Tanga,Tanzania.

    Klabu ya Yanga SC leo hii jioni imeibuka na ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Costal Union katika mchezo uliokwisha hivi punde katika dimba la Mkwawani jijini Tanga.

    Yanga ambayo wikendi iliyopita ilishindwa kufurukuta mbele ya klabu ya Ndanda FC imepata goli lake la ushindi kupitia kwa mlinzi na nahodha wake
    Nadir Haroub Cannavaro katika dakika ya 12 baada ya kuunganisha kwa kichwa mpira wa kulushwa wa mlinzi Mbuyu Twite.

    Kufuatia matokeo hayo Yanga imekwea kileleni ikiwa na alama 22 baada ya kucheza michezo 12 na kuishusha Azam FC mpaka nafasi ya pili ikiwa na alama 21 baada ya kushuka dimbani mara 11.

    Vikosi vilikuwa kama ifuatavyo....

    Coastal Union
    Shaaban Kado, Mbwana Hamisi, Sabri Rashid, Abdallah Mfuko, Juma Lui,Abdulhalim Humud, Joseph Mahundi/Said Mtindi, Godfrey Wambura, Hussein Sued, Rama Salim na Itubu Imbem.

    Yanga SC
    Ally Mustafa ‘Barthez’,Mbuyu Twite, Oscar Joshua, Rajab Zahir,Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Salum Telela,Simon Msuva, Said Juma ‘Kizota’, KpahSherman, Amisi Tambwe/Danny Mrwanda na Andrey Coutinho/Hussein Javu

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: VPL:YANGA YAIFUNGA COASTAL,CANNAVARO SHUJAA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top