London,England.
Mshambuliaji wa klabu ya Arsenal Mfaransa Olivier Giroud ameibuka mshindi wa shindano la kumsaka nyota wa soka mwenye mvuto zaidi (Handsome) katika ligi kuu ya England.
Shindano hilo lililoendeshwa na kampuni ya
mitindo na mavazi ya Paddy Power lililowatumia zaidi ya wanawake 250 kuchagua nyota 300 mwenye mvuto toka ligi kuu ya England na hapo ndipo nyota huyo alipoibuka kidedea huku nafasi ya pili ikienda kwa Santiago Vergini anayechezea Sunderland nafasi ya tatu ikienda kwa Matty James wa Leceister City.
Akiongea baada ya kukabidhiwa tuzo ya kioo cha dhahabu na kampuni ya Paddy Power,Giroud aliwashukuru wazazi wake kwa kumzaa akiwa na mvuto kisha wachezaji wenzie na mwisho timu yake wapiga picha wake pamoja na kinyozi wake.
Orodha ya wachezaji 11 wenye mvuto zaidi England hii hapa...
Fraizer Foster (Southampton), Santiago Vergini (Sunderland), Jason Shackell (Burnley), Erik Pieters (Stoke), Paul Konchesky (Leicester), Jesus Navas(Manchester City), Morgan Schneiderlin (Southampton), Matty James (Leicester),Nacer Chadli (Tottenham), Charlie Austin (QPR), Olivier Giroud (Arsenal).
0 comments:
Post a Comment