728x90 AdSpace

  • Latest News

    Friday, February 13, 2015

    HODGSON AMPIGIA HESABU HARRY KANE TIMU YA TAIFA


     Roy Hodgson

    London,England.


    Kocha wa timu ya taifa ya England Roy Hodgson amekiri kuwa anajipanga kumuita kwa mara ya kwanza kikosini mshambuliaji wa hatari wa Tottenham Harry Kane katika michezo miwili ya kimataifa itakayopigwa mwezi ujao dhidi ya Lithuania na Italy.
    Kane (21) amekuwa kwenye kiwango kizuri sana msimu huu ambapo mpaka sasa amefanikiwa kufunga jumla ya magoli 23 katika michezo
    35 amekuwa akitupiwa jicho na kocha huyo karibu kila mchezo uanoihusisha klabu ya yake.

    Ikiwa Kane ataitwa kikosini atakabiliwa na ushindani toka wa nyota wazoefu kama Wayne Rooney,Danny Welbeck na Danny Welbeck ambao kwa siku za hivi karibuni wamekuwa na mchango mkubwa.

    Mbali ya Harry Kane nyota wengine wanopigiwa chapuo kuitwa kikosini ni Danny Ings (Burnley), Charlie Austin (Queens Park Rangers) pamoja na Saido Berahino (West Brom)
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: HODGSON AMPIGIA HESABU HARRY KANE TIMU YA TAIFA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top