Barcelona,Hispania.
Lionel Messi ameshinda "hat-trick" yake ya 23 katika mechi 300 alizocheza ligi ya Hispania,La Liga, akiwa na timu yake ya Barcelona,wakati timu hiyo ikiichakaza Levante mabao 5-0 katika mchezo wa Jumapili usiku.
Matokeo hayo yanaonyesha kuwa Barcelona iko pointi moja tu nyuma ya vinara wa ligi hiyo, ambao waliichapa Deportivo La Coruna 2-0 Jumamosi.
Neymar ndiye aliyeanza kufungua kitabu cha magoli kwa Barcelona katika dakika ya 17,akifuatiwa na mvua ya magoli ya Messi katika dakika ya 38, 59 na 65 kabla ya Luis Suarez kukomelea msumari wa mwisho katika jeneza la Levante kwa kufunga bao linalotajwa kuwa goli bora la mechi hiyo.
Rekodi ya ufungaji ya Messi katika ligi kuu ya Hispania inaonyesha kuwa Mchezaji kutoka Argentina amefunga mabao 269 mpaka sasa katika mechi 300 lza ligi akifunga wastani wa magoli 0.89 kwa kila mchezo.
0 comments:
Post a Comment