728x90 AdSpace

  • Latest News

    Sunday, February 08, 2015

    YANGA YAMWAGA MIKATABA MIPYA KWA NYOTA WAKE

    Dar es salaam,Tanzania.

    Kutoka ndani ya klabu ya Yanga habari zinasema kuwa klabu hiyo imeanza kuwaongezea mikataba nyota wake ili kukwepa kuwapoteza katika dirisha lijalo la usajili.

    Taarifa za kuaminika zinasema tayari Yanga imeshamsainisha mkataba mpya wa miaka miwili mlinda mlango wake Deogratius Munishi "Dida" huku kiungo Haruna Niyonzima "Fabregas" akijiandaa kufuata nyazo za Dida baada ya mazungumzo kwenda sambamba.

    Baada ya Niyonzima itafuata zamu ya mlinzi Mbuyu Twite ambaye imeripotiwa kuna mambo kadhaa yanafanyiwa marekebisho katika mkataba wake wa sasa.

    Yanga wameamua kuanza mazungumzo mapema kutokana na umuhimu wa wachezaji hao katika timu ili wasije wakawapa nafasi wapinzani wao kuwasajili kwani muda uliobakia wanaruhusiwa kuzungumza na klabu nyingine.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: YANGA YAMWAGA MIKATABA MIPYA KWA NYOTA WAKE Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top