Uchambuzi na Mr Choi
KWA TAARIFA YAKO::
UEFA CHAMPIONS LEAGUE
PSG vs CHELSEA
22:45
PSG vs CHELSEA
22:45
Katika dimba la Parc des Princes vijana wa Laurent Blanc ambao wapo katika nafasi ya tatu ktk msimamo wa ligi kuu nchini Ufaransa watawakaribisha vinara wa ligi kuu nchini Uingereza Chelsea.
Ikumbukwe mtanange huu wa Uefa unatukubusha ule wa msimu uliopita ambapo timu zote zilitoka sare ya goli moja kwa moja huku Psg wakisawazisha kupitia Pastore baada ya Hazard kuipa Chelsea goli.
Kikubwa hasa si ukubwa wa vikosi vya timu zote hizi
bali ni ushindani uliyopo kwani hata pale darajan ni Ba aliye ikomboa Chelsea vinginevyo yangekuwa mengine.
Gumzo kubwa ni David Luiz ambaye alikipiga pale Chelsea kwa mafanikio huku akichukua ubingwa wa Uefa pale Munich (2012) na hivi sasa yupo Psg hivyo macho ya wengi ni kuona atakavyo cheza dhidi ya Chelsea pia tutaraji ubabe mwingi dhidi ya msaliti wa taifa la Brazil na kuhamia Spain si mwingine bali ni Costa kama unamuhusudu waweza muita Gavana.
Kuelekea mchezo huo kila timu ina wachezaji wazuri na inaweza kufanya lolote kulingana na watakavyo jipanga Chelsea watajivuna na Hazard,Fabregas na Costa lakini Psg kuna Ibra cadabra mchezaji mwenye magoli ya ajabu pia kuna Lavezzi,Cabaye na wengineo.
Swali ni Je!!Golini mwa Chelsea atasimama nani kati ya Cech na T.Courtois??
Ngoja tusubiri vita hivi vya Mourinho mwenye kiu ya kuchukua ubingwa huu akiwa na Chelsea.
NB::Psg wameanza kutumia uwanja wa Parc des Princes kama uwanja wao wa nyumbani tangu mwaka 1974.
Choikangta.ckt@gmail.com
T's up-0765 691418
T's up-0765 691418
0 comments:
Post a Comment