Radja:Klabu ya Manchester United imeripotiwa kutumia masaa machache yaliyobaki kabla dirisha la usajili halijafungwa ili kumsajili kiungo mzuiaji wa klabu ya As Roma Radja Nainggolan 26 mwenye thamani ya £30m.
Spurs:Klabu ya Tottenham hotspurs inasemekana inajiandaa kutumia kitita cha £60m ili kuwanasa nyota Yohan Cabaye,Aymeric Laporte na Jay Rodriguez kabla ya Feb 3.
Walcott:Klabu ya Arsenal inajiandaa kumpa mkataba mpya wa miaka mitano winga wake Theo Walcott 25 ili aendelee kubaki klabuni hapo.
Wilson:Klabu ya Manchester United inajiandaa kumpa mkataba mpya mshambuliaji wake kinda James Wilson 19 utakaomwezesha kutia kibindoni mshahara wa £20,000 kwa wiki.
Anderson:Kiungo wa klabu ya Manchester United Mbrazil Anderson kesho jumatatu anatarajiwa kufanyiwa vipimo vya afya na klabu ya Internacional ya nyumbani kwao kabla ya kutangazwa rasmi kuwa mchezaji wake mpya.Anderson atavuna £25,000 kama mshahara wa juma na £650,000 kama posho kwa mwaka.
Fletcher:Ndoto ya kiungo Darren Fletcher kuhamia Westham imekwama baada ya kushindwa kufikia makubaliano juu ya maslahi binafsi pamoja na ada ya uhamisho.
Coentrao:Vilabu vya Arsenal na Liverpool vimepewa kipaumbele na klabu ya Real Madrid kwa ajili ya kumsajili mlinzi wake wa kushoto Mreno Fabio Coentrao aliyeshindwa kupata namba ya kudumu katika kikosi cha kwanza cha kocha Carlo Ancelotti.
Lambert:Vilabu vya Hull City na QPR vimeripotiwa kuwa katika vita kali ya kumuwania kwa mkopo mshambuliaji wa Liverpool Ricky Lambert 31 kabla dirisha la usajili halijafungwa.
Dzeko:Kutoka ndani ya klabu ya Fernebahce habari zinasema klabu hiyo huenda ikafanya usajili wa kushitukiza wa mkopo wa mshambuliaji wa Manchester City Edin Dzeko ambaye aneripotiwa kujiandaa kumpisha Danny Ings toka klabu ya Barney.
Mourinho:Kocha Jose Mourinho huenda akaadhibiwa na chama cha soka cha England FA baada ya kukacha kuongea na vyombo vya habari katika mchezo wa jana wa ligi kuu dhidi ya Manchester City.
Reid:Klabu ya Liverpool imeripotiwa kujiandaa kutenga kitita cha £6.5m kwa ajili ya kuinasa saini ya mlinzi wa Westham Winston Reid 26.
0 comments:
Post a Comment