Mshambuliaji wa klabu ya Chelsea Diego Costa bado ameendelea kuonyesha kuwa yeye ni mtukutu baada ya kusema hatabadili aina ya uchezaji wake.
Costa 25 ambaye anatumikia adhabu ya kutocheza michezo mitatu kufuatia kufungiwa na chama cha soka cha England FA kwa kosa la kumkanyaga kwa makusudi kiungo wa Liverpool Emre Can amesema adhabu hiyo haitamfanya abadili aina ya uchezaji wake
"Mimi siyo malaika,huu ndiyo uchezaji wangu siku zote.Wanaosema mimi ni mgomvi nadhani wanautafsiri mpira tofauti"
Costa ameongeza kuwa hajioni kama ana hatia yoyote katika hilo nakusisitiza
"Mambo ya uwanjani huishia uwanjani.Mpira ukiisha tunapeana mikono na kila mtu anakwenda kwao.Sajawahi kumuumiza yoyote"
0 comments:
Post a Comment