728x90 AdSpace

  • Latest News

    Monday, February 02, 2015

    TFF:TUTAADHIBU WOTE WANAO AMINI USHIRIKINA

    Wakati dunia ya sasa katika soccer ikiamini kuwa ni mchezo wa kisayansi,unaotumia akili
    nyingi na nguvu kidogo, lakini bado dhana hiyo ni tofauti katika nchi kadha duniani na hasa barani Afrika.
    Vitendo vingi zimekuwa vikishuhudiwa vikiashiria uchawi au ushirikina katika soka kitendo ambacho kinalaaniwa kwa kurudisha nyuma maendeleo ya mchezo huo maarufu duniani.
    Kutokana na hilo, Shirikisho la mpira wa miguu nchini Tanzania (TFF) limesema vitendo vinavyoashiria
    ushirikina
    havitavumiliwa katika ligi kuu na timu zitaendelea kuhukumiwa kwa mujibu wa kanuni.
    Mkurugenzi wa mashindano wa TFF, Boniface Wambura amesema baadhi ya timu
    zimeadhibiwa kwa kuamini Imani za kishirikina katika jitihada za kutafuta ushindi.
    “Tumeshuhudia mara kadhaa kuona mchezaji,kiongozi au shabiki akifukia kitu uwanjani au
    sehemu ya goli kabla ya mechi “.
    “Wengine wakirusha ndege (njiwa) na baadhi ya timu zikigoma kutumia mlango wa
    kuingilia uwanjani au kugoma kuingia katika vyumba vya wachezaji kwa dhana potofu
    kuwa patakuwa na uchawi”, amesema Wambura.
    ‘Wakati mwingine, si vilabu, ni mashabiki,lakini kwa kufuata nembo za jezi zao, tunatoa
    adhabu”, alisema Kwa mujibu wa kiongozi huyo, kanuni za ligi
    zinatoa adhabu ya Sh500,000 (wastani wa dola 280) kwa kosa au kitendo kinachoashiria ushirikina.
    “Kinachofanyika, wakati mwingine sio ushirikina, ila kwa kuwa kuna watu ndio kazi
    yao, inabidi wafanye ili kuwaogopesha wachezaji wa timu pinzani kisaikolojia, lakini
    kwetu ni kosa pia”.
    Alisema kuna timu hivi karibuni iligoma kuingia chumba cha wachezaji na ilifanikiwa kushinda mechi na toka hapo timu nyingi zimekuwa na Imani hiyo.
    Vitendo vya ushirikina vimekuwa vikionekana katika ligi nyingi barani Afrika na TFF iliwahi
    kuzihukumu timu kubwa kama vile Simba na Yanga katika miaka ya nyuma kutokana na
    vitendo ambavyo aidha wachezaji au mashabiki walishiriki vikiashiria ushirikina.
    Lakini viongozi wengi, wakiwemo wa vilabu vya Simba na Yanga kwa wakati tofauti wamekuwa wakikana kujihusisha na vitendo
    hivyo wakisema ni potofu na havileti maendeleo katika mpira kwani ushindi unatokana na mazoezi.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: TFF:TUTAADHIBU WOTE WANAO AMINI USHIRIKINA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top