728x90 AdSpace

  • Latest News

    Thursday, February 05, 2015

    IVORY COAST YAIFUNGA CONGO NA KUTINGA FAINALI YA AFCON

    Timu ya Ivory Coast imefuzu kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika, AFCON, baada ya kuilaza Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo 3-1 katika nusu fainali ya kwanza iliyochezwa Jumatano usiku katika mji wa Bata.
                                                     

    Alikuwa nahodha wa Ivory Coast Yaya Toure aliyeanza kuwanyanyua
    mashabiki wa Ivory Coast alipofunga goli katika dakika ya 20 kutokana na mkwaju mkali na kumwaacha mlinda mlago wa DR Congo, Kidiaba, asijue la kufanya.

    DR Congo wakasawazisha bao hilo katika dakika ya 24 kwa njia ya penalti likifungwa na Mbokani Bezua.
    Gervinho akafunga bao la pili katika dakika ya 41. Hivyo hadi mapumziko Ivory Coast ilikuwa mbele kwa mabao 2-1.

    Kipindi cha pili timu hizo ziliendelea kushambuliana.
    Wilfried Kanon alikamilisha sherehe kwa timu yake ya Ivory Coast alipofunga bao la tatu katika dakika ya 68.
    Kwa matokeo hayo Ivory Coast imetinga fainali za michuano ya Afcon mwaka 2015, ambapo inamsubiri mshindi wa nusu fainali ya pili, kati ya Ghana na wenyeji Equatorial Guinea, Alhamisi
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: IVORY COAST YAIFUNGA CONGO NA KUTINGA FAINALI YA AFCON Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top