London,England.
Klabu ya Arsenal imeendeleza wimbi lake la ushindi baada ya leo kuizamisha klabu ya Aston Villa kwa jumla ya magoli 5-0 katika mchezo mkali wa ligi kuu uliopigwa katika dimba la Emirates.
Arsenal ilijipatia magoli yake kupitia kwa Oliver Giroud,Mesut Ozil,Theo Walcott,Santi Cazorla na kinda Hector Bellerin.
Katika mchezo wa pili vijana wa Southampton wameshindwa kuutumia vyema uwanja wao wa nyumbani wa St Mary's baada ya kukubali kichapo cha goli 1-0 toka kwa Swansea City.
Goli la Swansea limefungwa na kiungo wake Jonjo Shelvey katija dakika ya 83 huku Southampton wakimaliza wakiwa pungufu baada ya mlinzi wake Ryan Betrand kuonyeshwa kadi nyekundu kwa kumfanyia madhambi Modou Barrow wa Swansea.
Kufuatia matokeo hayo Southampton imebaki nafasi yake ya nne ikiwa na pointi 42 nafasi moja juu ya Arsenal kwa idadi nzuri ya magoli.
0 comments:
Post a Comment