London,England.
Kutoka gazeti la Daily Mail la nchini England habari zinasema kuwa klabu ya Arsenal inajipanga kumpiga bei kiungo wake Jack Wilshere katika dirisha lijalo la usajili barani Ulaya.
Dail Mail linaripoti kuwa Arsenal imechoshwa na tabia za kiungo huyo mwenye miaka 23 ambaye siku za hivi karibuni amekuwa akishindwa kujizuia na kujikuta akiendelea kubobea kwenye uvutaji wa sigara ambao mara kwa mara umekuwa ukimshushia heshima.
Arsenal pia imeonyesha kutoridhishwa na mchango wa kiungo huyo kutokana na kuwa majeruhi mara kwa mara kwani msimu huu pekee ameanza michezo saba tu ya ligi kuu.
Kutokana na ushindani mkubwa wa namba uliopo katika kikosi cha Arsenal haionekani kama Wilshere atapata nafasi mbele ya Aaron Ramsey,Santiago Cazorla,Mesut Ozil na Francis Coquelin.
Dail Mail limeendelea kutanabaisha kuwa Arsenal itamuuza kiungo huyo anayetia kibindoni mshahara wa £80,000 kwa wiki kwa ada ya £25m na vilabu vinavyo mtupia macho ni Liverpool na Westham United.
0 comments:
Post a Comment