728x90 AdSpace

  • Latest News

    Wednesday, February 04, 2015

    KILICHOMKOSESHA SAMATTA ULAJI CSKA HIKI HAPA

    Mshambuliaji wa TP Mazembe na Taifa Stars, Mbwana Samatta ameshindwa jaribio la kucheza soka Ulaya kwenye klabu ya CSKA Moscow ya Russia baada ya ofa yao kushindikikana kabla ya dirisha la usajili kufungwa.


    Mwezi uliopita, Samatta alikwenda kufanya majaribio ya kucheza soka kwenye klabu hiyo ya  Russia kwa siku saba na kufanikiwa, lakini
    mazungumzo baina ya CSKA na TP Mazembe yalikwenda taratibu na kukwamisha suala hilo.

    Akizungumzia suala hilo, Samatta alisema tatizo kubwa lililokwamisha dili hilo ni mawazo finyu ya klabu za Ulaya kwamba wachezaji wa Afrika ni wa bei rahisi, hivyo hata ofa waliyoitoa kwa klabu yake itakuwa ndogo.

    “Usajili ulifungwa mwisho wa Januari,dili lilitakiwa kukamilika kabla ya hapo lakini mambo yalikwenda ndivyo sivyo,tatizo wale walidhani nitakuwa mchezaji wa bei rahisi.

    “Tatizo jingine ni kwamba upepo
    unaonyesha bosi Moise Katumbi hataweza kuniruhusu kwa sasa, hata ikiwa hivyo lazima apokee fedha za maana,” alisemaSamatta.

    “Sijakata tamaa bado, nasubiri usajili wa dirisha kubwa nirudi tena kujaribu bahati, kuna klabu nyingine za Ubelgiji na nchi nyingine za Ulaya pia zimeonyesha nia.”

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: KILICHOMKOSESHA SAMATTA ULAJI CSKA HIKI HAPA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top