Azam imeingia makubaliano ya kusaini mkataba kati ya Azam Media na FUFA juu ya haki miliki za ligi kuu ya Uganda ambayo azamTV imedhamini ligi hiyo itakayotambulika sasa kama Azam Premier League.
Azam Media imeingia mkataba wenye thamani ya Dola za kimarekani zipatazo Milioni mbili sawa na fedha za kitanzania Bilioni 5.5.
Timu shiriki 16 zitapata
mgao wa Milioni 60 kwa mwaka, fedha ambazo zitazisaidia vilabu hivyo kujiendeleza zaidi na kumudu gharama za uendeshaji.
Historia mpya katika ramani ya mpira wa miguu imeandikwa Uganda leo, na ni matarajio yetu kuleta mabadiliko makubwa kama tufanyavyo Tanzania na VPL.
0 comments:
Post a Comment