Luanda,Angola.
Kiungo mshambuliaji wa zamani wa vilabu vya Barcelona,Ac Milan,Paris Saint Germain na timu ya taifa ya Brazil Ronaldinho 34 ameripotiwa kuwa karibu kutua katika klabu ya Kabuscorp inayoshiriki ligi ya Angola.
Ronaldinho ambaye kwa sasa anakipiga na klabu ya Queretaro
ya Mexico iliyomsajili kwa uhamisho wa miaka miwili na nusu mwezi septemba mwaka jana yuko katika hatua nzuri ya mazungumzo ya kutua Angola kupitia kwa wakala wake.
Akipasha habari hizo raisi wa klabu ya Kabscorp bwana Benedicto Kangamba amesema "Tuko katika mazungumzo na wakala wa mchezaji Ronaldinho kwa ajili ya kumsajili nyota huyo mshindi wa kombe la dunia.Matumaini ni makubwa kuwa tutamsajili"
"Tukiwa na mchezaji kama Ronaldinho naamini tunaweza kushinda ubingwa wa michuano ya kombe la ligi ya mabingwa Afrika na kisha kupata nafasi ya kucheza michuano ya vilabu bingwa duniani ambapo tutapimana ubavu na vilabu vya Ulaya"
Alimaliza raisi huyo ambaye klabu yake mwaka 2012 iliweka rekodi ya kumsajili nyota mwingine wa Brazil Rivaldo Boba Ferreirra.
0 comments:
Post a Comment