Golikipa wa timu ya Preston Thorsten Stuckmann ameeleza kuwa mshambuliaji Wayne Rooney alimuomba msamaha baada ya kuanguka katika eneo la hatari na kupata mkwaju wa penati.
Kipa huyo alimwangusha Rooney wakati
mchezaji huyo akielekea kufunga bao na kusababisha penati, Stuckmann, alisema "Rooney aliniomba msamahani na kuniambia ilikua ni nafasi yake ya kupata penati".
"Naamini tukio kama lile lingetokea kwenye goli la Manchester United toka kwa mshambuliaji wetu refa asingeweza kutupa penati sina shaka na hilo".
"Sisemi kama haikuwa penati, nachokisema hakukua na mgongano wowote"
Rooney alifunga mkwaju huo wa penati na kuipa timu yake ushindi mnono wa mabo 3-1dhidi ya Preston.
0 comments:
Post a Comment