Bale:Klabu ya Manchester United inapanga kutumia kitita cha €150m hapo majira ya joto kwa ajili ya kuwasajili nyota Gareth Bale toka Real Madrid na Matt Hummels wa Borussia Dortmund.
Simeone:Kocha Diego Simeone anatarajia kuendelea kuwepo katika klabu yake ya Atletico Madrid kwa kipindi kirefu baada ya kuripotiwa kuwa njiani kusaini mkataba mpya wa miaka mitano na kufuta uvumi wa kutimkia vilabu vya Manchester City ama Psg.
Gundogan:Baada ya Marco Reus kuamua kubakia Borussia Dortmund kiungo mwingine wa klabu hiyo Ilkay Gundogan naye ameripotiwa kuwa tayari kusaini mkataba mpya wa kuendelea kukipiga klabuni hapo.
Pogba:Klabu ya Arsenal imeripotiwa kuwa tayari kutoa kitita cha €100m kwa ajili ya kumnasa kiungo wa klabu ya Juventus Paul Pogba baada ya kiungo iliyekuwa ikimtaka kwa muda mrefu Morgan Schneiderlin kuanza kuwindwa na klabu ya Barcelona.
Martinez:Klabu ya Arsenal imeripotiwa kufikia makubaliano na klabu ya Porto kwa ajili ya kumsajili mshambuliaji hatari Mcolombia Jackson Martinez (28) kwa ada ya £29m.
De Bruyne:Klabu ya Manchester City imeripotiwa kuwa tayari kutoa pesa pamoja na mshambuliaji wake Edin Dzeko kwa ajili ya kuinasa saini ya kiungo wa klabu ya Wolfsburg Mbelgiji Kevin De Bruyne.
Hazard:Klabu ya Chelsea leo imekubali kumuuza kiungo wake Thorgan Hazard 21 kwenda klabu ya Borussia Monchengladbach lakini ikiwa na nafasi ya kumsajili tena kwa mara nyingine itakapo muhitaji.Thorgan ni mdogo wa winga Eden Hazard.
0 comments:
Post a Comment