Nusu fainali za pili za michuano ya
Kombe la Mataifa ya Afrika, Afcon kati ya Ghana na wenyeji Equatorial
Guinea zinaelezwa kama "ukanda wa vita" baada ya mchezo huo kusitishwa
kwa zaidi ya dakika 30 kwa sababu ya ghasia za mashabiki.
Mashabiki
kutoka majukwaani waliwarushia chupa za maji wachezaji, na kulazimisha
mashabiki wa Ghana kutafuta mahali pa kusitiri maisha yao nyuma ya goli,
polisi wa kuzuia ghasia na helikopta iliruka juu ya uwanja kuwatuliza
mashabiki lakini hawakufanikiwa.
"Ni kama sasa uwanja wa vita,"
kiliandika chama cha mpira cha Ghana(GFA) katika ujumbe wake wa tweeter,
kikidai kuwepo kwa vitendo vya "kinyama na uharibifu" na "mashambulio
ya vurugu kwa jambo lisilo na sababu" yalifanyika ndani ya uwanjani.
Wakati
mchezo unarejea, Ghana tayari ilikuwa imefunga magoli 3-0 na kutinga
fainali dhidi ya Ivory Coast itakayochezwa Jumapili. Kufika hatua hiyo
Ivory Coast, iliifunga DR Congo 3-1 katika nusu fainali ya kwanza
iliyochezwa Jumatano.
Vurugu zilikithiri katika kipindi cha pili cha mchezo kati ya Ghana na Equatorial Guinea.
Ushindi
huo wa Ghana haukuwafurahisha mashabiki wa timu mwenyeji, ambao
walikuwa na matumaini makubwa kuona timu yao inacheza fainali ya
Jumapili dhidi ya Ivory Coast.
Ghana ilianza kujipatia magoli yake
kupitia kwa Jordan Ayew akifunga katika dakika ya 42 kwa njia ya
penalti, Wakaso Mubarak dakika ya 45 na Andre Ayew alikipigilia msumari
wa moto katika dakika ya 75.
Goli hilo la tatu ndilo lililokuwa
limezidisha fujo kiwanjani kwa mashabiki wa Equatorial Guinea kuwarushia
chupa za maji wachezaji kiasi cha mpira huo kusimamishwa kwa muda
mrefu.
Kwa matokeo hayo Ivory Coast na Ghana ndizo zitakazocheza
fainali za Afcon kwa mwaka 2015 siku ya Jumapili zinazofanyika nchini
Equatorial Guinea na kutangazwa moja kwa moja na BBC.
Lakini
mchezo huo utatanguliwa na ule wa Jumamosi kutafuta mshindi wa tatu kati
Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo dhidi ya Equatorial Guinea
0 comments:
Post a Comment