Dar es salaam,Tanzania.
Baada ya kushindwa kupata ushindi katika michezo miwili mfululizo ya ligi kuu bara katika uwanja wa taifa klabu ya Yanga jioni ya leo imeibuka na ushindi wa goli 2-0 dhidi ya Mtibwa Sugar.
Mabadiliko yaliyofanywa na kocha Pluijim ya kumtoa Kpah Sherman na kumuingiza winga Mrisho Ngasa ndiyo yaliyo badili sura ya mchezo baada ya nyota huyo kufunga magoli mawili ya haraka haraka.
Ngasa alifunga goli la kwanza dakika ya 56 baada ya kumalizia krosi ya winga Simon Msuva aliyemzidi mbio mlinzi wa Mtibwa Vincent Andrew kabla ya kuongeza la pili dakika ya 66 baada ya kumlamba chenga mlinda mlango Said Mohammed.
Kufuatia matokeo hayo Yanga imerudi kileleni baada ya kufikisha pointi 25 ikufuatiwa na Azam yenye pointi 22.
Kikosi Yanga SC kilikuwa; Ally Mustafa ‘Barthez’, Mbuyu Twite, Edward Charles/Juma Abdul dk39, Rajab Zahir, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Salum Telela, Simon
Msuva, Haruna Niyonzima,Amissi
Tambwe, Kpah Sherman/Mrisho Ngassa dk53 na Andrey Coutinho/Hussein Javu dk83.
Mtibwa Sugar; Said Mohammed, Andrew Vincent, David Luhende, Ally Lundenga,Salim Mbonde, Shaaban Nditi, Ally Sharrif/
Ramadhani Kichuya dk62, Henry Joseph,Ame Ally, Ibrahim Rajab Jeba/Mohammed Ibrahim dk27 na Jamal Mnyate/Vincent
Barnabas dk60.
0 comments:
Post a Comment