Klabu ya Chelsea imeendelea kujichimbia kileleni mwa ligi ya Epl baada ya jioni hii kuibuka na ushindi wa goli 2-1 dhidi ya Aston Villa.
Ikicheza katika dimba la ugenini la Villa Park,Chelsea ilipata goli la kuongoza kupitia kwa winga wake Eden Hazard kufuatia krosi nzuri ya Oscar aliyeambaa na mpira wingi ya kulia.
Aston Villa ilijibu mapigo kwa goli la kichwa la mlinzi Jores Okore kufuatia krosi ya kiungo Carles Gil na kufuta ukame wa mabao uliodumu kwa dakika 659 sawa na masaa 11.
Chelsea ilipata goli lake la pili na la ushindi kupitia kwa mlinzi wake Branslav Ivanovic baada ya kutokea piga nikupige langoni mwa Villa.
Kufuatia ushindi huo Chelsea iko kileleni kwa alama 7 zaidi baada ya Manchester City kutoka sare ya goli 1-1 na Hull City.
Matokeo mengine ya Epl
Qpr 0-1 Southampton
Swansea 1-1 Sunderland
Leceister City 0-1 Crystal Palace
0 comments:
Post a Comment