728x90 AdSpace

Wednesday, June 21, 2017

Yanga yanawa mikono kwa Niyonzima,yasema haitakuwa naye msimu ujao


Dar Es Salaam,Tanzania.

KLABU ya Yanga kupitia kwa Katibu wake Mkuu,Charles Mkwasa imekiri kushindwa vita ya kumbakiza kikosini kiungo wake mahiri ,Mnyarwanda Haruna Niyonzima.

Mkwasa amesema Yanga haitaweza kuwa na Niyonzima msimu ujao baada ya kushindwa kufikia makubaliano ya mkataba mpya na kiungo huyo aliyedumu Jangwani kwa kipindi cha misimu sita.

Mkwasa ameongeza kuwa wameamua kumwachia Niyonzima licha ya kwamba  walikuwa bado wanamuhitaji kwa misimu miwili ijayo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 comments:

Post a Comment

Item Reviewed: Yanga yanawa mikono kwa Niyonzima,yasema haitakuwa naye msimu ujao Rating: 5 Reviewed By: Unknown