728x90 AdSpace

Tuesday, June 27, 2017

NGOMA AZITOSA YANGA,SIMBA ASAINI MIAKA MITATU SAUZI


Johannesburg,Afrika Kusini.

MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Zimbabwe, Donald Ngoma ameviacha kwenye mataa vilabu vya Simba na Yanga baada ya hii leo kujiunga na Polokwane City inayoshiriki ligi kuu nchini Afrika Kusini.

Ngoma mwenye umri wa miaka 27 amejiunga na Polokwane City kwa mkataba wa miaka mitatu baada ya kumaliza mkataba na mabingwa wa Tanzania, Yanga aliojiunga nao miaka miwili iliyopita akitokea FC Platinum ya nyumbani kwao Zimbabwe.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 comments:

Post a Comment

Item Reviewed: NGOMA AZITOSA YANGA,SIMBA ASAINI MIAKA MITATU SAUZI Rating: 5 Reviewed By: Unknown